Usiwachukie watu kwa sura zao,
Wapende watu kwa tabia zao.
Usiwaamini watu kwa kauli zao,
Washuhudie watu kwa matendo yao.
Usiwadharau watu kwa ufukara wao,
Waheshimu watu kwa utu wao.
Usiwajali watu kwa kipato chao,
Waheshimu watu kwa imani zao.
Usiwabeze watu kwa uduni wao,
Wahurumie watu kwa udhafu wao.
Mola atuwezeshe hayo,
Pia ziada ya kheri nyingine.
umesema vyema ndugu Mgaya. nashukuru kwa kukazia haya muhimu yatupasayo kama wanadamu.
ReplyDelete